Sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy amepata kuwa Mufti wa Tanzania kwa miongo miwili mpaka wakati wa kifo chake. .
Ahsante kwa maelezo yako kuhusu Sheikh Ali bin Hemed,babu yangu mzaa baba Al Marhum Sheikh Saidi bin Ali. Nimezingatia pia picha ya Al Marhum Sheikh Hemed bin Juma,aliyekuwa Mufti wa Tanzania bara na mwanafunzi mkubwa wa Sheikh Ali, je ! kuna chochote kitu kilichoandikwa kuhusu maisha yake ?
Assalaam. Mawaidha yapo, tafadhali wasiliana na watoto wake Al-Marhum Sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed; watoto hao ni Sheikh Mussa bin Hemed (0717 929057) na Sheikh Omar bin (Hemed 0713 226775).
A'alkm, kwenye vitabu vingi vya Sheikh Muhammd Kasim Mazrui, aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Kenya nimeona amemshirikisha shk Ali bin Hemed,na shk Abdallah Farsiy katka kuhakiki. Je shk Ali bin Hemed Albuhri ana kitabu chochote alichotunga? Na kama kipo kinaitwaje na naweza kukipataje?
Assalam Alaykum; itakuwa jambo jema yafanyike yafuatayo kama familia ya Sheikh Hemed wanaridhia: 1. Iandikwe historia ya Sheikh hapo kwa ufupi na iwekwe katika blog 2. Mawaidha yake yawekwe kwenye YouTube ili yaendelee kutuelimisha wengi
Sheikh Ali bin Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy
Tarehe na mahali alipozaliwa
Amezaliwa katika Kijiji cha Saadani, Tanga tarehe 29 August 1889 (sawa na Muharram 1307).
Sheikh Ali bin Hemed alilelewa na wazazi wake hapo Saadani na baadae wazazi wake wakahamia Kijiji cha Darigube kilichopo katika vijiji vya Maere na Kiwavu, Tanga.
Baba yake
Sheikh Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy - Maarufu Mwalimu "KIBAO".
Shughuli kubwa ya Baba yake ilikuwa Utabibu na Uandishi.
Pia aliandika vitabu vingi kama kitabu cha sharia za NIKAH na vinginevyo.
Tenzi hizi nyingi zilichukuliwa na J.W.T Allen kuzitafsiri kwa Kiingereza ambaye alipewa na Sheikh Muhammad bin Hemed, mwanawe Sheikh Hemed bin Abdallah. Tenzi hizi za familia ya Sheikh Hemed bin Abadallah sasa zimewekwa kwenye Maktaba za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mahali kwengineko kwenye tovuti tofauti tofauti za vyuo na za tafiti za Kiswahili.
Lakini pia ni nia pia ya mwandishi kuvitafuta vitabu hivi na kuviweka wazi kwa kila mtu kuweza kusoma na kuujua uwezo mkubwa wa uandishi aliokuwa nao A'ami yake Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy.
Mama yake
Bibi Maasimbu binti Mwinyimkuu bin Mwinyiamiri.
Kufa kwake
Ilikuwa Jumaapili tarehe 4 August 1957 siku ambayo aliendesha shughuli zake za kusomesha darsa zake kama kawaida mchana kutwa bila ya dalili zozote za dhahiri kwamba lipo tatizo la afya yake na kwamba mchana ule ndio ungekuwa mchana wake wa mwisho wa uhai wake duniani.Ilipofika usiku majira ya saa nne hivi aliingia ndani kulala.
Na huo siku hiyo ukawa mwisho wa umri wake duniani. Alifariki.
Alizikwa mchana wa Jumatatu tarehe 5 August 1957 katika kijiji kile kile alipozaliwa, yaani Saadani.
Ahsante kwa maelezo yako kuhusu Sheikh Ali bin Hemed,babu yangu mzaa baba Al Marhum Sheikh Saidi bin Ali.
ReplyDeleteNimezingatia pia picha ya Al Marhum Sheikh Hemed bin Juma,aliyekuwa Mufti wa Tanzania bara na mwanafunzi mkubwa wa Sheikh Ali, je ! kuna chochote kitu kilichoandikwa kuhusu maisha yake ?
Khelef Saidi Kibao
Salam Aleykum,
ReplyDeleteJe kuna mtu anayejuwa wapi ninaweza kupata mawaidha ya Mufti Hemed bin Juma bin Hemed.
Assalaam. Mawaidha yapo, tafadhali wasiliana na watoto wake Al-Marhum Sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed; watoto hao ni Sheikh Mussa bin Hemed (0717 929057) na Sheikh Omar bin (Hemed 0713 226775).
ReplyDeleteKaribu sana
Jazaka Allah kula khair, Insha Allah nitawasiliana nao.
ReplyDeleteAhsante Sana
A'alkm,
ReplyDeletekwenye vitabu vingi vya Sheikh Muhammd Kasim Mazrui, aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Kenya nimeona amemshirikisha shk Ali bin Hemed,na shk Abdallah Farsiy katka kuhakiki.
Je shk Ali bin Hemed Albuhri ana kitabu chochote alichotunga?
Na kama kipo kinaitwaje na naweza kukipataje?
Assalam Alaykum; itakuwa jambo jema yafanyike yafuatayo kama familia ya Sheikh Hemed wanaridhia:
ReplyDelete1. Iandikwe historia ya Sheikh hapo kwa ufupi na iwekwe katika blog
2. Mawaidha yake yawekwe kwenye YouTube ili yaendelee kutuelimisha wengi
darsa ya sheikh hemed zi wapi ? kama zipo tafadhali zitolewe
ReplyDeletedarsa ya sheikh hemed zi wapi ? kama zipo tafadhali zitolewe
ReplyDeletedarsa ya sheikh hemed zi wapi ? kama zipo tafadhali zitolewe
ReplyDelete