Asili ya Familia ya Sheikh Ali bin Hemed

Familia ya Sheikh Ali bin Hemed:
Asili hii imeanzia huko OMAN ya Kaskazini, Jimbo liitwalo Dhwaam, kutoka katika kijiji kinachoitwa Ghafur. Kijiji hiki cha Ghafur baadae kilivunjwa na kubaki mawe mawe tu. Jamaa wote waliokuwa wamebaki walihamia kijiji kingine kiitwacho Wadi Mestel ndani ya jimbo hilo hilo la Dhwaam.

Sheikh Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy ndiye aliyehama Oman na kuja kuanzisha makaazi Pemba akipitia Mombasa zaidi ya miaka mingi sana iliyopita. Mombasa alioa mke wa kabila la Mazrui, na kuzaa nae watoto. Mmoja ya watoto wake Sheikh Mas’uud bin Khelef bin Ali aliowazaa na mke huyu wa ki-Mazrui alikuwa ni Sheikh Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy.

Watoto wengine wa Sheikh Mas’uud bin Khelef bin Ali aliowazaa waliishi baina ya Pemba na Mombasa kwani hata Pemba alioa.

Mtoto huyu Sheikh Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali alioa Pemba. Nae akamzaa Sheikh Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy.

Sheikh Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali akakulia hapo na kuoa. Nae akamzaa Sheikh Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy

Sheikh Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali akakulia hapo Pemba na kuoa hapo. Nae akamzaa Sheikh Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali maarufu "Mwalimu Kibao"

Sheikh Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud (Mwalimu Kibao)nae akahamia Saadani (Tanga) na kumzaa Sheikh Ali bin Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy mnamo mwaka 1889 Muharram 1307.

Sasa yeye Sheikh Ali bin Hemed nae akaoa hapo na kuzaa watoto wote waliotajwa. Baadae nae akahamia Darigube-Tanga kutoka Saadani na kulea wanawe hapo. Wakati wa uhai wake Sheikh Ali bin Hemed aliendelea kuoa wake wengine baina ya Tanga mjini,Mnyanjani na nje ya Tanga pia kwa nyakati tofauti.
.

5 comments:

  1. Ah'sante nyingi sana kwa maalumati uliyo tupa juu ya as'li ya sheikh Ali (Mwenyezi Mugu akupe kila la kheri,kwani muda mrefu sana nilikuwa nikitafuta habari hizi hata katika Internet kubahatisha pengine kuna mtu anajuwa habari hizi.
    Soud bin Said bin Ali - Muscat Oman
    albuhriy28@yahoo.com

    ReplyDelete
  2. Nimesoma kwa uangalifu makala hii ya Asili ya Familia ya Al marhum Sheikh Ali bin Hemed.Kwa kuwa na mimi nilipata kusikia machache kuhusu haya kutoka kwa baadhi ya wanawe, kuna sehemu ambayo napenda kupata ufafanuzi zaidi, nayo ni hii; Sheikh Abdallah bin Said bin Abdallah alikuja TANGA (pengine Tongoni au Saadani)kwa shughuli za kibiashara na kuoa mwanamke wa kabila la ZIGUA (jina halikupatikana) ambaye ndiye mama yake Sheikh HEMED bin Abdallah (Mwalimu KIBAO)na sio kwamba alioa Pemba na kumzaa Mzee KIBAO.
    Pia kuhamia Mzee KIBAO Tanga kulitokana na sababu ya kutokukubalika kwake na baadhi ya nduguze wa Pemba ambao wengi wao walikuwa bado wana asili ya kiarabu tofauti na hivi sasa ambapo wengi wamechanganya na uafrika.Hivyo alihamia Saadani, Tanga, kuja kuishi na nduguze upande wa mama kwa kuwa hawakumtenga.
    Kama hivi ndivyo itakuwa ni vizuri sana kama asili ya familia ya upande wa kuukeni wa Al Marhum Sheikh Ali bin Hemed itajulikana kwani kilichopo katika maelizo haya ni jina la mama yake tu Bibi Masimbu binti Mwinyimkuu bin Mwinshehe bin Mwinyiamiri.

    Mwanafamilia Mfuatiliaji

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kabisa anayosema mwanafamilia mfuatiliaji.

    Kwa mujibu wa historia niliyosoma babu yake Hemed bin Abdulla - yaani Said bin Abdulla alikuwa ni Liwali wa Mtang'ata, kwa hivyo inaonyesha uhusiano wa hayo maeneo na ukoo huo.

    Bwana huyu alikuwa anachukuwa amri kutoka kwa Mazrui wa Mombasa wakati ule bado eneo hilo lilikuwa chini ya utawala wa Mazrui.

    Katika safari yake moja alipokuwa anatoka Mombasa kuelekea Tanga, alipigwa mkuki wa sumu na Sultani wa Wadigo na kufariki akiwa njiani.

    Hii inatoka kwenye kitabu cha Sh. Al Amin Mazrui na alimtaja kabisa kwa jina na uhusiano wake na Sh. Ali bin Hemed (kwamba he was his great grandfather).

    Inawezekana huyu Mzee alikuwa na mke mmoja Tanga na mwengine Pemba. Pemba kwa wakati ule ilikuwa chini ya utawala wa Mazrui wa Mombasa vile vile.

    Mjukuu wa Ali bin Hemed

    ReplyDelete
  4. Asalam Alaikum...Naomba kama itawezekana kutupatia anuwani ya kitabu cha Sh.AlAmin Mazrui ambapo ameelezea habari ya Abdullah bin Said bin Abdullah na uhusiano wa Sh.Ali

    Note: Sh. Said Al-Mughaeri Mtungaji wa kitabu JUHAINA AL'AKHAR FI TAREH ZINJIBAR (kitabu kinaelezea makabila ya warabu wa kioman ambao wanaishi east africa) ameeleza juu ya Sh.Hemed na baadae mtoto wake Sh.Ali nakwamba walifikia cheo cha (WALI) Tanga enzi za wagerumani,bila ya maongezo zaidi.
    Kitabu kimetung'wa kwa kiarabu na kimechapishwa na Ministry of Heritage and Culture of Oman.

    Soud Al-buhriy Muscat Oman.
    albuhriy28@yahoo.com

    ReplyDelete
  5. Katika kitabu زجبار شخصيات واحداث by Nassor Abdullah Al-riyami,pengine inawezekana the title kwa english kuwa kama hivi:[Zanzibar,personalities and events] published 2009. katika kitabu hicho ameeleza habari ya Alamin Ali mazrui na ametaja baadhi ya wanafuzi wake waliokuwa maarufu na mmoja wao alikuwa Ali bin hemed, na mwandish wa kitabu amemtaja kwa kwa kuazia neno or designation [Al-alama] العلامة على بن حميد البحرى lakab hiyo enaazia kabla ya jina la mwenyeelimu kubwa na hasa katika elimu ya dini. # kitabu hicho kime nunuliwa sana Oman na hasa wasomaji waliokuwa hawana fikra ya kutosha ya alaka baina Oman and east africa.

    Soud Al-buhriy Muscat Oman.
    albuhriy28@yahoo.com

    ReplyDelete