.
Asili ya Familia ya Sheikh Ali bin Hemed
Familia ya Sheikh Ali bin Hemed:
Asili hii imeanzia huko OMAN ya Kaskazini, Jimbo liitwalo Dhwaam, kutoka katika kijiji kinachoitwa Ghafur. Kijiji hiki cha Ghafur baadae kilivunjwa na kubaki mawe mawe tu. Jamaa wote waliokuwa wamebaki walihamia kijiji kingine kiitwacho Wadi Mestel ndani ya jimbo hilo hilo la Dhwaam.
Sheikh Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy ndiye aliyehama Oman na kuja kuanzisha makaazi Pemba akipitia Mombasa zaidi ya miaka mingi sana iliyopita. Mombasa alioa mke wa kabila la Mazrui, na kuzaa nae watoto. Mmoja ya watoto wake Sheikh Mas’uud bin Khelef bin Ali aliowazaa na mke huyu wa ki-Mazrui alikuwa ni Sheikh Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy.
Watoto wengine wa Sheikh Mas’uud bin Khelef bin Ali aliowazaa waliishi baina ya Pemba na Mombasa kwani hata Pemba alioa.
Mtoto huyu Sheikh Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali alioa Pemba. Nae akamzaa Sheikh Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy.
Sheikh Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali akakulia hapo na kuoa. Nae akamzaa Sheikh Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy
Sheikh Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali akakulia hapo Pemba na kuoa hapo. Nae akamzaa Sheikh Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali maarufu "Mwalimu Kibao"
Sheikh Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud (Mwalimu Kibao)nae akahamia Saadani (Tanga) na kumzaa Sheikh Ali bin Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy mnamo mwaka 1889 Muharram 1307.
Sasa yeye Sheikh Ali bin Hemed nae akaoa hapo na kuzaa watoto wote waliotajwa. Baadae nae akahamia Darigube-Tanga kutoka Saadani na kulea wanawe hapo. Wakati wa uhai wake Sheikh Ali bin Hemed aliendelea kuoa wake wengine baina ya Tanga mjini,Mnyanjani na nje ya Tanga pia kwa nyakati tofauti.

Maulid ya kukutanisha watoto, wajukuu, vitukuu na vilembwe vya Sheikh Ali bin Hemed - anayesoma ni Sheikh Abdallah "Magomeni"
Kila ufikapo mfungo sita, familia ya Sheikh Ali bin Hemed hukutana na kufanya maulid ya kusherekea uzawa wa Mtume Muhammad (SAW), na pia kuchukua fursa hiyo kukutanisha watoto, wajukuu, vitukuu na vilembwe vya Sheikh Ali bin Hemed, kukaa pamoja na kutambuana.
Sehemu ya watoto, wajukuu na vitukuu vya Sheikh Ali bin Hemed
Sheikh Mussa bin Hemed bin Jumaa bin Hemed akiongoza duaa baada ya swala.
Sheikh Khelef bin Said bin Ali bin Hemed akitambulisha nduguze, na watoto wao.
Sheikh Khelef bin Said bin Ali bin Hemed akitambulisha wanawe
Sheikh Mussa bin Hemed bin Jumaa bin Hemed akimtambulisha nduguye na wanawe.
A'ami Masoud bin Ali bin Hemed akitambulisha familia yake
A'ami Nassor bin Ali bin Hemed akitambulishwa akiwa pamoja na familia yake na A'ami Issa
Watoto, wajukuu na wakwe waliooa kwa Al-Marhum Sheikh Muhammad bin Ali bin Hemed
A'ami Issa bin Ali bin Hemed akitambulisha familia yake
Sehemu ya familia ya A'ami Zuheri bin Ali ikijitambulisha.
Familiya Al-Marhum Sheikh Salim bin Ali ikijitambulisha
A'ami Hashil Abdallah Hashil naye akitambulisha familia yake
Vitukuu na Vilembwe vya Al'Marhum Sheikh Hemed bin Ali
Watoto wa Al-Marhum A'ami Kahlan bin Ali wakitambulishwa na A'ami Issa
Watoto wa Al-Marhum A'ami Hemed Muhammad Hemed (Maarufu A'ami Kwame) wakitambulishwa na A'ami Issa.
.
Mwana wa nduguye Sheikh Ali bin Hemed - Sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed Al-Buhriy
Wanawe Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy
Mwanawe Sheikh Ali bin Hemed - Zuheri bin Ali

Mwanawe Sheikh Ali bin Hemed - Madina bint Ali

Mwanawe Sheikh Ali bin Hemed - Sheikh Issa bin Ali

Mwanawe Sheikh Ali bin Hemed - Sheikh Hemed bin Ali

Mwanawe Sheikh Ali bin Hemed - Sheikh Salim bin Ali
Mwanawe Sheikh Ali bin Hemed - Sheikh Kehlan bin Ali

Mjukuu na Kitukuu wakitoa hadithi za babu yao Sheikh Hemed bin Abdallah
Mjukuu Sheikh Zuheri bin Ali bin Hemed na Kitukuu Sheikh Ali bin Hemed Ali Hemed wakielezea moja ya hadithi za A'ami yake Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy.
.
.
Vitabu alivyotunga Sheikh Ali bin Hemed
Hii ilikuwa ni kusahihisha tafsiri ya Qur'aan iliyotolewa na Makadiani
.
Wanazuoni wenzake na wanafunzi wake
Wanazuoni waliokuwa pamoja na yeye hapa Tanga wakati wake ni:
1. Sheikh Ayub bin Khamis Al-Kamadhy
2. Sheikh Dhikri bin Said
3. Sheikh Kinero
4. Sheikh Toba
5. Sheikh Suleiman wa Petukiza
Wanafunzi wake wakubwa:
Wanafunzi wake ni wengi wa mjini Tanga na waliotoka miji mbalimbali kuja kusoma kwake. Lakini baadhi ya wanafunzi wake wakubwa waliokuwa wakijulikana kwa ilimu yao ni:
1. Sheik Amir bin Jumaa Al-Bimani
2. Sheikh Muhammad bin Ayub Al-Kamadhy
3. Sheikh Suleiman bin Mbwana
4. Sheikh Muhammad bin Dhikri
5. Sheikh Muhammad bin Ali bin Hemed (Mwanawe)
6. Sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed (Mwana wa nduguye)
Hawa wote waliotajwa wamefariki, lakini ilimu zao na za Sheikh wao zinaendelea. Alhamdulillah.
..

Kazi alizofanya Sheikh Ali bin Hemed
- Kwa ilimu yake alikubalika na kuadhimishwa Afrika Mashariki yote. Alipata kuwa Kadhi wa Tanga kuanzia mwaka 1339 Hijriah "1921" mpaka mwaka 1354 Hijriah "1935".Na aliendelea kufanya kazi nyingine za Serikali zilizokamatana na mas'ala ya dini.
- Alisomesha wanafunzi wengi wa mjini Tanga na waliokuja kutoka miji ya nje ya Tanga
- Amesafiri sana miji ya bara kwa ajili ya Tabligh ya dini na alikuwa ni mwenye sauti ya kusikiwa na kila mwenye kuhudhuria.
- Ametunga vitabu vingi vya lugha ya Kiswahili na harfu za kizungu.
Katika vilivyotangaa zaidi ni kitabu chake cha Mirathi pamoja na mas'ala ya Wasiya na Hibba.
Alikamilisha kukiandika kitabu hiki mwezi wa Septemba 1923 na kikapitiwa na kupasishwa na Sayid Ahmad bin Sumeyt na Sheikh Twahir bin Abubakar, Kadhi wa Zanzibar. - Kitabu hiki cha Mirathi kilitafsiriwa kwa lugha ya Kiingereza na Bwana Philip Mitchell aliekuwa Bwana Shauri (Administrative Officer) wakati huo Tanganyika.
Lakini pia kitabu hiki kilitumiwa sana katika Mahakama za Sheria, Afrika Mashariki, kila panapotokea haja ya kufutu mas'ala ya mirathi kwa mujibu wa sharia ya Kiislamu. - Kitabu kingine kilichotangaa zadi ni "Taarifu Juu ya Tafsiri ya Wakadiani" alichokitowa mwaka 1954.
Kitabu hiki kinabainisha uwongo wa Makadiani katika tafsiri yao ya Qur'ani waliyoitoa mwaka 1953 - Vile vile alianza kuandika tafsiri ya Qur'ani kwa lugha ya Kiswahili kwa kutumia harfu za Kiarabu.
Mwenyiezi Mungu hakumjaalia umri wa kuweza kuikamilisha kazi hiyo. Alifariki baada ya kukamilisha tafsiri ya Suratul-An'aam.
Tafsiri hiyo ambayo mwenyewe ameipa jina la "Al-Murshidul-Kariim Ilaa Tafsiyril-Qur'anil-Adhiim", inaandikwa tena lakini kwa kutumia harfu za kizungu ili itabiishwe na Waislam wapate kuisoma na kunufaika.
Kazi hiyo ya kuandika tena kwa harfu za kizungu inafanywa na mwanawe Zuheri bin Ali bin Hemed.
Masomo yake - Sheikh Ali bin Hemed
- Alianza masomo ya Qur'ani hapo kijijini Saadani akisomeshwa na Mwalimu Kadhi Mwinchande.Masomo ya awali ya ilimu ya dini alianza akusomeshwa na baba yake Mzee Hemed bin Abdallah. Pia alihudhuria masomo ya shule, Tanga School, na kusitisha masomo ya shule akiwa darasa la pili ili aendelee na masomo ya dini.
- Aliendelea na masomo yake ya dini kwa Sheikh Faqih (kutoka Magunyani na kuishi Mafere, Muheza - Tanga). Alisomeshwa na Sheikh huyu Rubu'ul Ibadah).
- Alisoma ilimu ya Faraidh (Mirathi) kwa Sheikh Khamis bin Salim Riyamy wa Tanga. Sheikh Khamis alikuwa Kadhi wa Tanga.
- Vilevile alisoma tena ilimu ya Faraidh na ilimu ya Nahau kwa Sheikh Umar bin Stambuli bin Abubakar As-Saady wa Tanga. Sheikh Umar alikuwa Kadhi wa Tanga.
- Kisha akaenda Unguja kuzidi kuongeza ilimu yake. Akasoma hapo Unguja kwa Kadhi Sayid bin Abubakar bin Sumeyt. Vile vile akasoma kwa Sheikh Abdallah bin Muhammad Bakathir.
Akazidi kuongeza ilimu yake ya Faraidh kwa kusomeshwa na Sheikh Salim bin Said bin Seif Ash-Sheheyby ambae alikuwa ndiye mjuzi wa ilimu ya Urithi zama hizo kuliko mwanachuoni yeyote mwengine wa pande hizi. - Vile vile hapo Unguja alisoma ilimu ya Balagha na Mantiq kwa Sheikh Abubakar bin Abdallah Bakathir (Huyu ni mtoto wa Sheikh Sheikh Abdallah Bakathir).
- Lakini mwanachuoni, kama tajiri, hakinai kwa alichopata, hutaka kila siku kuongeza. Kwa hiyo alikwenda Mombasa kwa Sheikh Al-Amin bin Ali Mazrui akachukuwa aliyoyachukuwa. Ilimu ya Miqaat aliisomea huko.
Aila yake
Wake zake waliomkalia eda:
Alipata kuwa na watoto 22 (Sio kwa mpangilio maalum)
Wajukuu na vutukuu vyake itoshe tu kusema kwamba idadi yao ni kubwa. (Updated 1st Oct 2017)
- Bibi Mwanaasiya bint-Ishaaq
- Bibi Khadija bint Khamis (Bibi Lulu)
- Bibi Saumu bint Mwin'dadi
- Bi Mkubwa Swalehe (Bi Mkubwa) - Mama yake Sheikh Said Ali
- Bi Akida wa Mnyanjani- Huyu bibi hakuzaa nae na kumuacha na aliolewa tena Mombasa na kumzaaa Sheikh Shariff Athuman - Majengo Mombasa
- Asia binti Ishaq (Bi Mwanasia)
- Halima bint Salim (Mama yao akina Kibibi, Suleiman na Khelefu)
- Fatuma Jumbe (Bi Victoria) - Hakuzaa nae
- Mwana Huba (Mama Maasimbu)- alifariki akiwa kwenye treni
- Khadija binti Khamis (Bi Lulu)
- Fatuma Kiziwa - Mama yake Zaituni bint Ali
- Asha binti Suleiman - Mama yake Kahlani
- Saumu binti Mwindadi - Hakuzaa nae
- Bibi Mweni - Hakuzaa nae
- Bi Hindie - Hakuzaa nae
- Bi Fatuma Kiziwa
- Bi Mwanajumbe - Hakuzaa nae
- Bi Halima wa Pangani - Hakuzaa nae
- Mama yake Rashid "Makoko" bin Ali wa Kilosa.
- Bibi Zania Mohamed Magambo - Hakuzaa nae
- Mwana Hawa (Mama yake Mwanaarabu bint Ali)
- Bi Fatuma Mbegu - Hakuzaa nae
- Bi Mwanahawa binti Nassor Kyamba (Mama yake Mwanahawa)
- Alioa pia huko Bweni, Pangani - Jina kamili pia halijaweza kupatikana
Wake zake kwa ujumla: (Mpangilio usio sahihi)
Alipata kuwa na watoto 22 (Sio kwa mpangilio maalum)
- Said bin Ali - Amezaliwa 1912 - Amefariki 26th February 1988
- Hemed bin Ali - Amezaliwa (tarehe) - Amefariki 8th January 1966
- Nassor bin Ali - Amezaliwa (tarehe) - Amefariki (tarehe)
- Rashid bin Ali - Amezaliwa (tarehe) - Amefariki (tarehe)
- Abdallah bin Ali - Amezaliwa (1923) - Amefariki (1956)
- Mohammed bin Ali - Amezaliwa 27th February 1927 - Amefariki 6th December 1995
- Khelef bin Ali - Amezaliwa (tarehe) - Amefariki (tarehe)
- Swaleh bin Ali - Amezaliwa 1929 - Amefariki March 2005
- Salim bin Ali - Amezaliwa 22nd August 1933 - Amefariki 16th January 1999
- Suleiman bin Ali - Amezaliwa (tarehe) - Amefariki (tarehe)
- Masoud bin Ali - Amezaliwa 3rd August 1944
- Zuheri bin Ali - Amezaliwa 11th November 1944 - Amefariki 13 September 2015
- Nassor bin Ali - Amezaliwa 22nd May 1947
- Kahlan bin Ali - Amezaliwa 1st January 1949 - Amefariki (tarehe)
- Muhsin bin Ali - Amezaliwa 12th December 1950
- Issa bin Ali - Amezaliwa 5th July 1955
- Zaitun bint Ali - Amezaliwa (tarehe)
- Maasimbu bint Ali - Amezaliwa (tarehe) - Amefariki (tarehe)
- Kibibi bint Ali - Amezaliwa (tarehe) - Amefariki (tarehe)
- Zalfa bint Ali - Amezaliwa (tarehe) - Amefariki (tarehe)
- Mwanaarabu bint Ali - Amezaliwa 10th August 1945
- Madina bint Ali - Amezaliwa 13th June 1953
- Watoto sita (6) walifariki yeye akiwa hai.
- Watoto tisa (9) wamefariki baada ya yeye kufariki.
- Watoto saba (7) bado wako hai (wanne wa kiume na watatu wa kike) - August 2010
Wajukuu na vutukuu vyake itoshe tu kusema kwamba idadi yao ni kubwa. (Updated 1st Oct 2017)
Wake zake Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy
Subscribe to:
Posts (Atom)