Mjukuu wa nduguye Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy; Mwanahamisa bint Hemed bin Muhammad Hemed Al-Buhriy

Al-Marhum Mwanahamisa bint Hemed bin Muhammad bin Hemed Al-Buhriy amefariki Tarehe 21 May 2017

Mjukuu wa Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy; Mwalimu Muhammad bin Said bin Ali bin Hemed Al-Buhriy

Al-Marhum Mwalimu Muhammad bin Said bin Ali bin Hemed Al-Buhriy amefariki tarehe 12 May 2017

Mjukuu wa Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy; Mwalimu Ali bin Hemed bin Ali bin Hemed Al-Buhriy

Al-Marhum Mwalimu Ali bin Hemed bin Ali bin Hemed Al-Buhriy amefariki tarehe 22 November 2015

Mwanawe Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy; Al-Marhum Sheikh Zuheri bin Ali Al-Buhriy

Al-Marhum Sheikh Zuheri bin Ali Al-Buhriy amefariki tarehe 13 September 2015 sawa na Mfungo 2, tarehe 28, Mwaka1436



Maulid ya kukutanisha watoto, wajukuu, vitukuu na vilembwe vya Sheikh Ali bin Hemed (2014)


Baadhi ya watoto wa Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy


Baadhi ya watoto wa Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy wakiwa na Mjuku wa Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy


Maulid yakiendelea




Wajukuu, Vitukuu na Vilembwe vya Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy




Sheikh Khelef Bin Said Bin Ali Al-Buhriy akiongoza darsa fupi kwa niaba ya akina-Ammi kwa waliohudhuria


Ali bin Masoud bin Ali Hemed Al-Buhriy akimtambulisha A'ami, Mama yake, familia yake wakiwa na nduguye na watoto wao


Aami Nassor bin Ali Hemed Al-Buhriy akitambulisha familia yake


Aami Issa bin Ali Hemed Al-Buhriy akimtambulisha mwanawe

Maulid ya kukutanisha watoto, wajukuu, vitukuu na vilembwe vya Sheikh Ali bin Hemed (2013)

Baadhi ya watoto wa Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy

Baadhi watoto wa Al-Marhum Sheikh Ali bin Hemed Al-buhriy katika picha ya pamoja wakiwa Dar es Salaam baada kumaliza kusoma Maulid ya kuwarehemu "Amwaat" mwaka 2013 na kuwa pamoja na kufahamiana.

Zaitun bint Ali bin Hemed Al-Buhriy akitambulisha wajukuuze ambao ni vituku kwa Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy


Ali bin Masoud bin Ali Hemed Al-Buhriy akimtambulisha A'ami na Mama yake wakiwa na nduguze na watoto wao


Shariff Abdallah akimtambulisha Mama yake Shangazi Mwanaarabu bint Ali Hemed Al-Buhriy; akiwa na nduguze na watoto wao


Familia ya Sheikh Nassor bin Ali Hemed Al-Buhriy ikijitambulisha akiwa na watoto wake


Shangazi Madina bint Ali bin Hemed Al-Buhriy akijitambulisha


Familia ya Sheikh Issa bin Ali Hemed Al-Buhriy ikijitambulisha akiwa na watoto wake


Ayoub bin Muhammad Hemed Al-Buhriy akitambulisha nduguze na watoto wao


ZamZam bint Said Ali Hemed Al-Buhriy akitambulisha nduguze na watoto wao


Asiya bint Muhammad Ali Hemed Al-Buhriy akitambulisha nduguze na watoto wao


Sheikh Mussa bin Hemed bin Jumaa bin Hemed Al-Buhriy akitambulisha wajukuu na vilembwe vya Bi Mganga bint Hemed Al-Buhriy ambaye ni dadie Sheikh Ali bin Hemed Al-buhriy


Sheikh Mkoye (Mume wa Batuli bint Salim) akimtambulisha mama, watoto na wajukuu wa Sheikh Salim bin Ali Hemed Al-Buhriy


Ali bin Zuheri Ali Hemed Al-Buhriy akitambulisha nduguze, Shemejie na watoto wao


Ali bin Kahlan Ali Hemed Al-Buhriy akitambulisha nduguze na watoto wao


Nassor bin Matuga (Kitukuu cha Sheikh Hemed bin Ali bin Hemed Al-Buhriy) akimtambulisha mama yake (Mjukuu wa Sheikh Hemed bin Ali bin Hemed Al-Buhriy) nduguze na watoto wao


Wasomaji wa taarifa za Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy wameomba kupata maisha na shughuli zaidi za watoto na mtoto wa nduguye Sheikh Ali ili nao waweze kunufaika zaidi

  • Sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed - ukusanyaji wa tarifa zake unaendelea.
  • Sheikh Muhammad bin Ali bin Hemed - ukusanyaji wa tarifa zake unaendelea.
  • Sheikh Salim bin Ali bin Hemed - ukusanyaji wa tarifa zake unaendelea.

  • Picha ya Sheikh Salim bin Ali bin Hemed Al-Buhriy


    Moja ya wasomaji wetu aliomba kuona walau picha ya Sheikh Salim bin Ali bin Hemed Al-Buhriy, mtoto wa Sheikh Ali akiwa katika shughuli zake za kushona. Aliye pamoja nae ni rafiki yake Sheikh Salim bin Ali akijulikana kama Harub.

    Moja ya Picha za Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy


    Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy


    Hii ni moja ya picha chache Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy alizokuwa akikubali kupigwa, kwani alikuwa hapendi. Hapa amesimama nyumba ya pili barabara 13

    .

    Asili ya Mama yake Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy



    Aliekuja Mtang'ata kutoka mji wa Jimbo, sehemu za Vanga, ni Sheikh Mwinyiamiri bin Khatibu Baamiry. Sheikh Mwinyiamiri aliongozana na nduguye Bi Mwanangazija pamoja na mkewe Bi Mwakanda - walizaa watoto watano (5) akiwamo Bi Mganga.

    Bi Mganga aliolewa na Sheikh Abdallah bin Said bin Abdallah bin Masoud na kuzaliwa Sheikh Hemed bin Abdallah bin Said Al-Buhriy (Mwalimu Kibao).

    Kaka yake Bi Mganga binti Mwinyiamiri, yaani Mwinyimkuu bin Mwinyiamiri nae alizaa watoto wanne (4) akiwamo Bi Maasimbu. Bi Maasimbu aliolewa Saadani na Sheikh Hemed bin Abdallah bin Said Al-Buhriy mbao ni ni ndugu shangazi kwa Mjomba.

    .

    Familia ya Sheikh Masoud Al-Buhriy tokea alipohama Oman miaka zaidi ya 200 iliyopita - ikiwa mpaka na wajukuu wa Sheikh Ali bin Hemed



    Kama ambavyo nilivyoelezea hapo punde, kuhusu Sheikh Masoud Al-Buhriy alivyohama kutoka Oman kuja Pemba, lakini akianzisha makaazi kwanza Mombasa-Kenya. Hii picha ni mitiririko wa familia yake akianzia yeye mwenyewe.
    Bonyeza picha- yaani "double click" ili ipate kufunguka kwa ukubwa.


    1. A'ami Nassor bin Ali mkubwa - Hakuna taarifa kama alioa

    2. A'ami Rashid bin Ali - Aliwahi kukaa Kilosa. Utafiti juu ya wanawe huko unaendelea

    3. A'ami Abdallah bin Ali - hakuwahi kuoa

    4. A'ami Khelef bin Ali- Alifariki akiwa mdogo

    5. A'ami Suleiman bin Ali - Alifariki akiwa mdogo

    6. Shangazi Maasimbu binti Ali- Hakuwahi kuzaa ingawa aliwahi kuolewa na Sheikh Amir bin Jumaa Al-Bimani

    7. Shangazi Kibibi binti Ali- Alifariki akiwa mdogo

    8. Shangazi Zalfa binti Ali- Alifariki akiwa mdogo


    Wasomaji na Wafuatiliaji wa Blog hii, kama kuna maboresho katika chati hii nitashukuru kupata maoni yenu.
    .