Asili ya Mama yake Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy



Aliekuja Mtang'ata kutoka mji wa Jimbo, sehemu za Vanga, ni Sheikh Mwinyiamiri bin Khatibu Baamiry. Sheikh Mwinyiamiri aliongozana na nduguye Bi Mwanangazija pamoja na mkewe Bi Mwakanda - walizaa watoto watano (5) akiwamo Bi Mganga.

Bi Mganga aliolewa na Sheikh Abdallah bin Said bin Abdallah bin Masoud na kuzaliwa Sheikh Hemed bin Abdallah bin Said Al-Buhriy (Mwalimu Kibao).

Kaka yake Bi Mganga binti Mwinyiamiri, yaani Mwinyimkuu bin Mwinyiamiri nae alizaa watoto wanne (4) akiwamo Bi Maasimbu. Bi Maasimbu aliolewa Saadani na Sheikh Hemed bin Abdallah bin Said Al-Buhriy mbao ni ni ndugu shangazi kwa Mjomba.

.

No comments:

Post a Comment