Mjukuu Sheikh Zuheri bin Ali bin Hemed na Kitukuu Sheikh Ali bin Hemed Ali Hemed wakielezea moja ya hadithi za A'ami yake Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy. .
Sheikh Ali bin Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy
Tarehe na mahali alipozaliwa
Amezaliwa katika Kijiji cha Saadani, Tanga tarehe 29 August 1889 (sawa na Muharram 1307).
Sheikh Ali bin Hemed alilelewa na wazazi wake hapo Saadani na baadae wazazi wake wakahamia Kijiji cha Darigube kilichopo katika vijiji vya Maere na Kiwavu, Tanga.
Baba yake
Sheikh Hemed bin Abdallah bin Said bin Abdallah bin Mas’uud bin Khelef bin Ali bin Said bin Nassor bin Suleiman Al-Buhriy Al-Hinaiy - Maarufu Mwalimu "KIBAO".
Shughuli kubwa ya Baba yake ilikuwa Utabibu na Uandishi.
Pia aliandika vitabu vingi kama kitabu cha sharia za NIKAH na vinginevyo.
Tenzi hizi nyingi zilichukuliwa na J.W.T Allen kuzitafsiri kwa Kiingereza ambaye alipewa na Sheikh Muhammad bin Hemed, mwanawe Sheikh Hemed bin Abdallah. Tenzi hizi za familia ya Sheikh Hemed bin Abadallah sasa zimewekwa kwenye Maktaba za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mahali kwengineko kwenye tovuti tofauti tofauti za vyuo na za tafiti za Kiswahili.
Lakini pia ni nia pia ya mwandishi kuvitafuta vitabu hivi na kuviweka wazi kwa kila mtu kuweza kusoma na kuujua uwezo mkubwa wa uandishi aliokuwa nao A'ami yake Sheikh Ali bin Hemed Al-Buhriy.
Mama yake
Bibi Maasimbu binti Mwinyimkuu bin Mwinyiamiri.
Kufa kwake
Ilikuwa Jumaapili tarehe 4 August 1957 siku ambayo aliendesha shughuli zake za kusomesha darsa zake kama kawaida mchana kutwa bila ya dalili zozote za dhahiri kwamba lipo tatizo la afya yake na kwamba mchana ule ndio ungekuwa mchana wake wa mwisho wa uhai wake duniani.Ilipofika usiku majira ya saa nne hivi aliingia ndani kulala.
Na huo siku hiyo ukawa mwisho wa umri wake duniani. Alifariki.
Alizikwa mchana wa Jumatatu tarehe 5 August 1957 katika kijiji kile kile alipozaliwa, yaani Saadani.
No comments:
Post a Comment