Mwanawe Sheikh Ali bin Hemed - Al-Marhum Sheikh Muhammad bin Ali


.

2 comments:

  1. Sh. Mohammed Ali alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Bakwata.

    Alikuwa na elimu kubwa sana juu ya mambo ya sheria ya dini ya Kiislamu. Hii aliipata kutoka kwa baba yake. Vile vile alikuwa na library kubwa sana ya vitabu vya dini.

    Aliwahi kuniambia mwenyewe kwamba alitunga kitabu kinachohusu mambo ya mirathi ya kiislamu au sheria za kiislamu lakini hakuruhusiwa kukichapisha kwa vile hakuwa na digrii ya Sheria. Kitabu hicho ilibidi kichapishwe Zanzibar na kitoke kwa jina la mtu mwengine ambaye alikuwa Jaji (nadhani Sh. Said Dahoma kama sikukosea maana miaka imekuwa mingi).

    Hilo ndilo lililomsukuma Sh. Mohammed kwenda kusomea digrii ya sheria wakati akiwa na umri mkubwa. Ijapokuwa alipata shida lakini Mwenyezi Mungu alimjaaliwa kufanikiwa na kupata digrii yake.

    Mjukuu wa Ali bin Hemed

    ReplyDelete
  2. mbona sijaona Zuheri Ali akitajwa japo pahala pamoja....

    ReplyDelete