- Alianza masomo ya Qur'ani hapo kijijini Saadani akisomeshwa na Mwalimu Kadhi Mwinchande.Masomo ya awali ya ilimu ya dini alianza akusomeshwa na baba yake Mzee Hemed bin Abdallah. Pia alihudhuria masomo ya shule, Tanga School, na kusitisha masomo ya shule akiwa darasa la pili ili aendelee na masomo ya dini.
- Aliendelea na masomo yake ya dini kwa Sheikh Faqih (kutoka Magunyani na kuishi Mafere, Muheza - Tanga). Alisomeshwa na Sheikh huyu Rubu'ul Ibadah).
- Alisoma ilimu ya Faraidh (Mirathi) kwa Sheikh Khamis bin Salim Riyamy wa Tanga. Sheikh Khamis alikuwa Kadhi wa Tanga.
- Vilevile alisoma tena ilimu ya Faraidh na ilimu ya Nahau kwa Sheikh Umar bin Stambuli bin Abubakar As-Saady wa Tanga. Sheikh Umar alikuwa Kadhi wa Tanga.
- Kisha akaenda Unguja kuzidi kuongeza ilimu yake. Akasoma hapo Unguja kwa Kadhi Sayid bin Abubakar bin Sumeyt. Vile vile akasoma kwa Sheikh Abdallah bin Muhammad Bakathir.
Akazidi kuongeza ilimu yake ya Faraidh kwa kusomeshwa na Sheikh Salim bin Said bin Seif Ash-Sheheyby ambae alikuwa ndiye mjuzi wa ilimu ya Urithi zama hizo kuliko mwanachuoni yeyote mwengine wa pande hizi. - Vile vile hapo Unguja alisoma ilimu ya Balagha na Mantiq kwa Sheikh Abubakar bin Abdallah Bakathir (Huyu ni mtoto wa Sheikh Sheikh Abdallah Bakathir).
- Lakini mwanachuoni, kama tajiri, hakinai kwa alichopata, hutaka kila siku kuongeza. Kwa hiyo alikwenda Mombasa kwa Sheikh Al-Amin bin Ali Mazrui akachukuwa aliyoyachukuwa. Ilimu ya Miqaat aliisomea huko.
Masomo yake - Sheikh Ali bin Hemed
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment